Skip to main content

Maswali Yanayoulizwa Sana

Maswali Yanayoulizwa Sana

Hujapata unachotafuta?

Angalia Kituo cha Usaidizi ili upate usaidizi zaidi wa kiufundi.

Je, Outline ni VPN?

Hapana, Outline si VPN. Inamruhusu mtu yeyote kuweka mipangilio na kudhibiti seva yake mwenyewe ya VPN ya faragha.

Kwa nini ni vigumu zaidi kuzuia Outline ikilinganishwa na VPN za kawaida?

Outline hutumia itifaki isiyo ya mashauriano na isiyofanana na chochote ambayo ni vigumu kutambuliwa, kinyume na itifaki za VPN za kawaida ambazo zinaweza kutambuliwa na kuzuiwa kwa urahisi.

Utoaji wa faragha wa idhini ya kufikia. Tofauti na VPN za umma, ambazo zana ya kuzuia tovuti inaweza kufikia na kuorodhesha kwa urahisi seva inazotaka kuzuia.

Ukitumia Outline ni rahisi kuunda upya seva ikizuiwa.

Nilipakua Programu ya Outline lakini sina ufunguo. Nitapata wapi ufunguo?

Funguo zinaweza tu kuzalishwa kwenye Outline Manager. Wasiliana na mtu unayemfahamu ambaye ameweka mipangilio ya seva kwa kutumia Outline Manager, au uweke mipangilio ya seva yako mwenyewe kisha ujitumie ufunguo.

Je, Outline ni salama?
Outline imekaguliwa na kampuni mbili huru za usalama. Soma ripoti zao hapa: Radically Open Security (Machi 2018, Desemba 2022), Cure53 (Desemba 2018, Januari 2024).
Nina wasiwasi kuhusu data yangu. Mnakusanya taarifa zipi?
Outline haikusanyi taarifa binafsi isipokuwa ukichagua kuzitoa. Outline pia haikusanyi maelezo kuhusu tovuti unazotembelea au watu unaowasiliana nao wala mambo mnayowasiliana kuhusu. Ili usome zaidi kuhusu data tunayokusanya, angalia makala haya ya usaidizi. Ikiwa unafungua au kuingia katika akaunti ukitumia mtoa huduma za wingu kupitia Outline Manager, hatupati taarifa zozote unazotoa kwa mtoa huduma za wingu, kama vile anwani ya barua pepe, jina, maelezo ya kulipa na maelezo yako ya malipo.
Nitachaguaje mtoa huduma za wingu?

Chagua mtoa huduma za wingu kulingana na bajeti na mahitaji yako binafsi. Google na Amazon Web Services ni kampuni za kuaminika. Digital Ocean inatoa baadhi ya mipango ya bei nafuu zaidi kwa mwezi na watumiaji wengi wameripoti kuwa ni rahisi zaidi kuweka mipangilio yake.

Nitashirikije ufunguo?

Unaweza kushiriki funguo moja kwa moja kwenye Outline Manager. Hatua ya kubofya sehemu ya CTA (mwito wa kuchukua hatua) ya kushiriki ufunguo itaonyesha mwaliko wenye ujumbe uliojazwa kiotomatiki unaompa mpokeaji maagizo ya jinsi ya kukubali ufunguo, kupakua Programu Teja na kuunganisha kwenye seva yako ya Outline. Unahitaji kujua anwani ya barua pepe au nambari ya simu ya mpokeaji wako ili uweze kumtumia ufunguo na maagizo ya kuunganisha.

VPN nyingi hazilipishwi. Kwa nini nilipe kutekeleza VPN yangu mwenyewe kwa kutumia Outline?

Kwenye VPN nyingi zisizolipishwa, huwezi kujua ni nani anayeweza kufikia data yako. VPN nyingi zisizolipishwa hushiriki au kuuza data yako au kufuatilia shughuli zako za mtandaoni. Baadhi ya wataalamu wa usalama wanadai kuwa VPN nyingi maarufu zisizolipishwa huruhusu serikali au wapelelezi wengine wafikie data kwa njia fiche. VPN nyingi zisizolipishwa pia zinaweza kuzuiwa na kutambuliwa.

Je, ninaruhusiwa kutumia au kuiga chapa ya Outline?
Ingawa Outline ni programu huria na inatumika bila malipo, chapa yetu inamilikiwa na Jigsaw na haipaswi kutumiwa vibaya. Tafadhali soma na ufuate mwongozo huu wa watumiaji ili kuhakikisha kwamba unaepuka madai yanayopotosha au kuharibu uhusiano wako na Outline au Jigsaw na hutumia kwa usahihi vipengele vya chapa vilivyoidhinishwa.
Je, nani anamiliki na kudumisha Outline?

Mnamo 2026, umiliki wa Outline ulihamishiwa kwa Outline Foundation, shirika huru lisilolenga faida. Outline ilizinduliwa mwaka 2018 na Jigsaw, kitengo cha Google kinachobuni teknolojia ibuka. Outline inaendelea kuwa mradi huria usiolipishwa unaostawi kutokana na michango ya jumuiya.

Hujapata unachohitaji?

Wasiliana na timu ili upate usaidizi zaidi

Wasiliana nasi