Jinsi Inavyofanya Kazi
Tekeleza VPN yako mwenyewe na udhibiti trafiki yako ya intaneti
Outline huboresha muundo wa VPN za asili kwa kufanya iwe rahisi kwa mtu yeyote kubuni VPN yake mwenyewe.
VPN za Asili
Mara nyingi, ni rahisi kuzuia VPN za asili kwa sababu zinatambulika kwa urahisi.
Unapotumia VPN, trafiki yako haikutambulishi, lakini itifaki fulani za usalama zinazotumiwa na VPN maarufu hutumia sahihi za kipekee za kriptografia ambazo zinaweza kutambuliwa na kuzuiwa kwa urahisi.
Unapounganisha kifaa chako kwenye VPN ya asili, trafiki yako inaweza kutambuliwa kwa urahisi kwa sababu ukubwa wa trafiki sawa huifanya rahisi kupata na kuzuia seva.
Outline
Outline hufanya kazi wakati VPN nyingine zimezuiwa na haiwezi kuathiriwa na mbinu changamano za kuweka vizuizi kama vile uzuiaji kwenye mtandao au uzuiaji wa IP.
Outline ni thabiti zaidi kwa sababu imetengenezwa kwa kutumia itifaki ambayo imebuniwa hivi kwamba ni vigumu kuitambua na hivyo ni vigumu kuizuia.
Shiriki kwa faragha idhini ya kufikia seva yako na kikundi cha watu unaowaamini. Idadi ndogo ya watu waliounganisha kwenye seva yako inamaanisha kuwa ni vigumu zaidi kuitambua na rahisi kuwa ya faragha.
Outline ilibuniwa kwa kuzingatia faragha yako.
Kamwe haihifadhi kumbukumbu ya trafiki yako wala kufuatilia matumizi yako ya intaneti.
Jipatie Outline Manager Jipatie Programu ya Outline