Anza
Bidhaa Mbili Zinazofanya Kazi Pamoja
Outline ina bidhaa mbili zinazohusiana ambazo hufanya kazi pamoja kukupa wewe na jumuiya yako uwezo wa kufikia intaneti bila kukatizwa.
Step 1
Anza na Outline Manager
Weka mipangilio ya seva yako ukitumia programu ya Outline Manager ya kompyuta za mezani
Pakua programu ya Outline Manager ya kompyuta za mezani ili uanze kuweka mipangilio ya seva yako. Tulibuni Outline ili kukuwezesha kudhibiti kila kitu kuhusu seva yako katika sehemu moja. Chagua kwenye orodha ya watoa huduma za wingu wanaoaminika, au unaweza kutumia miundomsingi yako mwenyewe ya Linux. Huduma nyingi za wingu hutoa mipango kwa USD $5 kwa mwezi au bei nafuu zaidi.
Baada ya kupakua Outline Manager, utaombwa uchague huduma ya wingu unapotaka kuendesha seva yako. Chagua miongoni mwa watoa huduma wanaoaminika zaidi kama vile Digital Ocean, AWS au Google Cloud. Baada ya kuchagua huduma ya wingu unayotaka kuitumia, watakuelekeza kwenye mchakato wao wa kuanza kutumia, lakini utaweza kudhibiti seva yako kwenye Outline Manager.
Outline inakuruhusu kuchagua mahali unapotaka seva yako iwe. Tuma trafiki yako ipitie Singapore, Ujerumani au Marekani, miongoni mwa maeneo mengine mengi.
Step 2
Zalisha Funguo
Zalisha funguo ili uunganishe vifaa vyako na uwape walio kwenye mtandao wako idhini ya kufikia
Baada ya kuweka mipangilio ya seva yako, zalisha funguo za kipekee moja kwa moja kwenye programu ya Outline Manager ya kompyuta za mezani. Outline Manager hukuwezesha kutuma mialiko ya kuunganisha kwenye seva yako kupitia mfumo wa mawasiliano unaoupendelea. Funguo ndizo zinazotumika kuunganisha vifaa vyako kwenye Outline Manager na kuvilinda kwa kutumia seva yako. Kila ufunguo ni wa kipekee na unaweza kuudhibiti au kuufuta moja kwa moja kwenye seva. Vikomo vya data hukuwezesha kudhibiti kipimo data ambacho kila ufunguo unaruhusiwa kutumia.
Kuunganisha kwenye seva yako ni rahisi kama kukubali mwaliko wako. Ukishaunganishwa, unaweza kuwasha au kuzima muunganisho wako kwa urahisi ukitumia programu hiyo.
Step 3
Jipatie Programu ya Outline ya kompyuta za mezani na vifaa vya mkononi
Unganisha kwa kutumia ufunguo wako wa kipekee
Pakua Programu ya Outline kwenye App store au Duka la Google Play, kisha uunganishe kwa kutumia ufunguo wako wa kipekee. Programu ya Outline inapatikana kwenye vifaa vya mkononi na kompyuta za mezani, kwa hivyo unaweza kufikia intaneti wazi na kuwasiliana kwa faragha popote ulipo na kwenye vifaa vyako vyote.
Baada ya kuunganisha vifaa vyako mwenyewe, unaweza kuwapa marafiki au wafanyakazi wenzako idhini ya kufikia seva yako. Zalisha funguo za kipekee kisha umtumie mtu yeyote katika mtandao wako anayehitaji kufikia intaneti bila kukatizwa. Tumia vikomo vya data kudhibiti ufikiaji wa seva yako. Hali hii inakupa chaguo la kudhibiti matumizi endapo mtu fulani katika mtandao wako anatumia kipimo data cha juu sana.
Tumia kiungo mbadala. Fahamu masharti ya kutekeleza programu teja.